Jumanne 16 Septemba 2025 - 14:33
Hijra Iliyoigeuza Qum Kuwa Mji Mkuu wa Kiimani kwa Iran

Hawza/ Hijra ya Bibi Fatima al-Ma‘suma (a.s.) kwenda Qum ilikuwa mwanzo wa mageuzi makubwa katika historia ya Iran; uwepo mfupi lakini wenye athari zilizoendelea kwa karne nyingi, Qum, kwa baraka ya kaburi lake tukufu, ikageuka kuwa moyo unaodunda wa Ushi‘a na chemchemi ya kuenea kwa utamaduni wa Ahlul-Bayt (a.s.) kote Iran na katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, kutokana na kumbukumbu ya tarehe 23 Rabi‘ al-Awwal – siku ya kuwasili kwa baraka za Bibi mtukufu Fatima al-Ma‘suma (a.s.) katika mji wa Qum – tunabainisha kwamba uwepo wake huo wa muda mfupi ulileta mageuzi makubwa katika historia ya Iran, Qum, kwa baraka za kaburi lake tukufu, ikawa kitovu cha elimu na imani cha Ahlul-Bayt (a.s.) na ikachukua jukumu kubwa mno katika kueneza Ushi‘a.

Nafasi ya Bibi al-Ma‘suma (a.s.) katika Kueneza Ushi‘a Iran

Hijra ya Bibi Fatima al-Ma‘suma (a.s.) kutoka Madina kwenda Qum ni nukta muhimu mno katika historia ya Ushi‘a nchini Iran, Ingawa alikaa Qum kwa takribani siku kumi na saba tu, baraka za uwepo na mazishi yake ziliifanya Qum kuwa kitovu cha elimu na imani kwa Mashia; mji ambao baadaye ulijulikana kama “Ummu al-Qura ya Shia.”

Hijra Iliyoandika Historia

Hijra ya Bibi al-Ma‘suma (a.s.) ni miongoni mwa hijra mashuhuri za karne moja ya Shia, kuanzia nusu ya karne ya pili hadi nusu ya karne ya tatu Hijria, na ina nafasi ya pekee, Kama ilivyokuwa hijra ya Imam Ridha (a.s.), hijra hii pia ilisababisha Iran kuchukua sura mpya na kugeuza mwelekeo wake wa kiutamaduni kuelekea mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.) [1][2][3].

Qum; Moyo Unaodunda wa Ushi‘a

Kuanzia mwanzo, kwa baraka ya kaburi la Bibi al-Ma‘suma (a.s.), Qum ikawa kimbilio la waumini na hifadhi ya wanazuoni na wapokezi wa hadithi, ushauri wa mara kwa mara wa Maimamu (a.s.) kuhusiana na fadhila za kumzuru Bibi huyu mtukufu ulidhihirisha hadhi yake kubwa, miongoni mwa hadithi zilizopokewa ni:

“Atakayemzuru binti yangu mjini Qum, Pepo itapasa yeye.”

“Atakayemzuru dada yangu mjini Qum, Pepo itakuwa wajibu kwake.”

“Atakayemzuru shangazi yetu mjini Qum, Pepo itamlazimu.”

Hadithi hizi ziliwafanya maelfu ya Mashia kusafiri hadi Qum kwa ajili ya ziara, na wengi wao wakaamua kuishi humo, hivyo basi, Qum haraka ikawa moja ya miji yenye wageni wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu na ngome kuu ya Ushi‘a [4][5].

R'azi Qazwini, katika karne ya sita Hijria, aliandika: “Kaburi la Bibi al-Ma‘suma (a.s.) linatembelewa na kila mmoja, hata wafalme na watawala wa Hanafiyya na Shafi‘iyya huutafuta ukaribu wa Mwenyezi Mungu kwa kulitolea heshima.” [6].
Aidha, vyanzo vya karne ya nne vimeripoti ujio wa watu kutoka Rayy na maeneo mengine kwa ajili ya kumzuru Bibi huyu mtukufu [7].

Eneo la Jibal na Athari ya Qum kwa Miji iliyopo pembizoni

Katika vyanzo vya kihistoria, jina “Jibal” lilitumiwa kuashiria eneo kubwa lililojumuisha miji kama Isfahan, Zanjan, Qazwin, Hamadan, Dinawar, Rayy na Kermanshah [11]. Qum, iliyoko katikati ya eneo hili, kwa baraka ya kaburi la Bibi al-Ma‘suma (a.s.), ikawa kitovu cha uenezaji wa mafundisho ya Shia na taratibu ikaathiri miji yote ya jirani.

Wanahistoria wameandika kuwa kuenea kwa Ushi‘a katika miji kama Rayy na K'ashan kuliathiriwa moja kwa moja na Qum na wanazuoni wake [8][9][10].
Safari za wafanyabiashara, mazuwari na wanafunzi wa elimu kati ya miji hiyo na Qum, ziliunda njia ya kupitisha fikra na tamaduni za Kishia, hata miji iliyo mbali kijiografia na Qum, kama baadhi ya sehemu za Kerman, ilipokea mafundisho ya Kishia kupitia uhusiano wa kielimu na kiutamaduni na mji huu.

Nafasi ya Ash‘ari na Wapokezi wa hadithi wa Qum

Katika kipindi hicho, ukoo wa Ash‘ari ulikuwa na nafasi kubwa ndani ya Qum na walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Maimamu (a.s.) [12].
Mamia ya wapokezi wa hadithi na wanafunzi wa Ahlul-Bayt walihudhuria Qum, na hivyo kuhifadhi na kusambaza urithi wa hadithi za Shia [13].
Mazingira haya yaliifanya Qum kuwa chanzo kikuu cha kuimarisha Ushi‘a katika eneo lote la Jibal na hatimaye katika sehemu kubwa ya Iran [14][15].

Hawza ya Qum; Urithi wa Bibi al-Ma‘suma (a.s.)

Miongoni mwa matunda makubwa ya uwepo wa Bibi al-Ma‘suma (a.s.) Qum ni kuanzishwa kwa Hawza ya kielimu ya mji huu, ripoti zinaonyesha kuwa katika karne ya nne Hijria, zaidi ya wanazuoni 200,000 walikuwepo katika Qum [16].

Bidii za kielimu za wanazuoni wa Qum zilisababisha kuandikwa kwa mamia ya vitabu, ambavyo vingi vilisafirishwa hadi vituo vingine vya kielimu vya Kiislamu na kuchukua nafasi muhimu katika kueneza Ushi‘a [17].
Mfano maarufu ni kitabu "Mi’atu Manqaba" kilichoandikwa na Ibn Shadhan Qummi, ambacho kilifundishwa ndani ya Msikiti Mtakatifu wa Haram [18].

Hitimisho:
Hijra na mazishi ya Bibi Fatima al-Ma‘suma (a.s.) Qum yalisababisha mji huu kuwa mhimili mkuu wa Ushi‘a nchini Iran, Qum haikubaki tu katika kueneza mafundisho ya Kishia katika eneo la Jibal na miji jirani kama Rayy, Kashan, Aveh na Farahan, bali pia ilieneza ushawishi wake hadi maeneo ya mbali kama Kerman.

Kwa baraka ya hadithi nyingi za Maimamu (a.s.) kuhusu fadhila ya kumzuru, Qum ikawa kituo cha kudumu cha Waislamu wa Kishia, kutoka katika kitovu hiki kuliibuka Hawza yenye ushawishi mkubwa wa kielimu na kiutamaduni ambayo kwa karne nyingi imekuwa kinara wa kusambaza elimu na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.) katika ulimwengu mzima, bila shaka, siri ya uimara na uimarikaji wa Ushi‘a nchini Iran ipo katika baraka ya uwepo wa Bibi Fatima al-Ma‘suma (a.s.).

Rejea:
1. Tareekh Qum, uk. 308; Khulasat al-Buldan, uk. 117.

2. Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu Qum – Karne ya 3 Hijria, uk. 128.

3. Hareem Mutahhar Bibi wa Heshima ya Ahlul-Bayt Bibi al-Ma‘suma (a.s.), Dibaji ya Ustadh Dawani, uk. 34.

4. Tareekh Qum, uk. 309–311; Bihar al-Anwar, juz. 99, uk. 265; Zad al-Ma‘ad, uk. 547.

5. Maelezo Kuhusu Qum na Bibi al-Ma‘suma (a.s.), uk. 228.

6. al-Naqd, uk. 588.

7. Tareekh Qum, uk. 308.

8. Tareekh Qum, uk. 318–319; Kashan Katika Njia ya Ushi‘a, uk. 120–124; Historia ya Kuenea kwa Ushi‘a Rayy, uk. 32.

9. Historia ya Ushi‘a Iran Kuanzia Mwanzo Hadi Karne ya 9 Hijria, uk. 117–132.

10. Mahusiano ya Ahlul-Bayt na Wairani, uk. 195; Maelezo Kuhusu Qum, juz. 5, uk. 363–364.

11. Yaqut al-Hamawi, Mu‘jam al-Buldan, juz. 2, uk. 99.

12. Vinara wa Kwanza wa Ushi‘a Iran, uk. 56.

13. Historia ya Ushi‘a Iran Kuanzia Mwanzo Hadi Mwisho wa Karne ya 9 Hijria, uk. 308.

14. Historia ya Iran Katika Karne za Mwanzo za Kiislamu, uk. 326.

15. Qum-Nameh, uk. 143.

16. Majlisi, Lawami‘ Sahib-Qirani, juz. 1, uk. 478.

17. Jabari, Madrasa ya Hadithi ya Qum, uk. 108.

18. Kanz al-Fawa’id, juz. 2, uk. 55; Da’irat al-Ma‘arif Kubra ya Kiislamu, juz. 4, chini ya “Ibn Shadhan,” uk. 52–53.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha